Latest News

Leicester City mabingwa wapya EPL


Klabu ya soka ya Leicester City wameshinda taji la ligi kuu England katika historia inayovutia kwenye ligi hiyo. Suluhu ya 2-2 waliyoipata Tottenham dhidi ya Chelsea siku ya jumatatu usiku ilisababisha mafanikio hayo makubwa kuwahi kutokea kwa upande wa Claudio Ranieri.
Leicester walianza kampeni zao za ubingwa huku wakipewa nafasi moja tu kati ya 5000 kushinda taji la ligi na pia wakitoka katika janga la kutaka kushuka daraja.
Lakini wamepoteza michezo mitatu tu katika kile kinachotafsiriwa kama hadithi za kale na ushindi wa kipekee katika timu hiyo. Wapinzani wao wa karibu Spurs,Arsenal,Manchester City, Manchester United na washindi wa ligi msimu uliopita Chelsea wameshindwa kuwazuia mbweha katika msimu mzima wa ligi.

Washindi wapya

1
Leicester City ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza mara ya kwanza kabisa
  • 5,000-1 uwezekano wao wa kushinda ligi msimu ulipoanza
  • 2-2 matokeo ya mechi kati ya Chelsea na Tottenham ambayo iliwazawadi Leicester taji la ligi
Getty
Rais wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino amesema historia nzuri ya Leicester ilikua ni kama hadithi za kale.

No comments:

Post a Comment

PERUZI24HOURS Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.