Abiria wametakiwa kuondoka kwa
dharura kutoka ndege ya shirika la Ryanair iliyokuwa safarini
kuelekea
Manchester, Uingereza kutokana na tishio la bomu.
Baadaye ilibainika kwamba hakukuwa na bomu.
Abiria wawili ambao tabia yao ilikuwa imewafanya watu kuwashuku walizuiliwa na polisi kwa muda lakini baadaye wakaachiliwa.
Taarifa zinasema wasiwasi ulizuka baada ya wanaume hao wawili kusikiza wakijibizana kwa sauti na mmoja wao akataja neno “bomu”.
Polisi wamesema hali ya kawaida imerejea nalo shirika la ndege la Ryanair likasema ndege hiyo itaondoka na abiria karibuni.
Kisa hicho kimetokea saa chache baada ya watu kulazimishwa kuondoka uwanja wa michezo wa Old Trafford, Manchester Jumapili baada ya kitu kilichohofiwa kuwa bomu kuonekana.
Baadaye ilibainika kwamba kilikuwa kifaa kilichoachwa na kampuni iliyokuwa ikifanya mazoezi ya kiusalama ikitumia mbwa wa kunusa.
No comments:
Post a Comment