Latest News

Yanga haitaki mazoea FA



YANGA jana ilifuzu nusu fainali za michuano ya kombe la Shirikisho, FA kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Prisons katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuungana na Simba, Mbao na Azam katika hatua ya nusu fainali ambayo droo yake itachezeshwa leo. Yanga imepata ushindi huo ikitoka kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika ilipotupwa nje kwa jumla ya mabao 4-1 na MC Alger ya Algeria.
Mabingwa hao watetezi wa kombe hilo walianza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 15 kupitia kwa mshambuliaji wake Mrundi Amisi Tambwe. Tambwe alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Geofrey Mashiuya.
Bao hilo lilikuwa kama mkosi kwa Prisons kwani mchezaji wake Jeremiah Juma alilazimika kutoka katika dakika ya 16 na nafasi yake kuchukuliwa na Victor Hangay. Yanga iliandika bao la pili katika dakika ya 40 kupitia kwa Obrey Chirwa na safari hii mtengenazaji wa bao hilo akiwa Mwashiuya tena.
Simon Msuva aliifungia Yanga bao la tatu dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili akifunga kwa shuti kali nje ya 18. Hangay alikuwa na nafasi ya kuipatia timu yake Prisons bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penalti lakini mkwaju aliopiga uligonga mwamba na mpira kuwahiwa na mabeki wa Yanga waliouondosha eneo la hatari.
Mwamuzi wa mechi hiyo aliwapa Prisons penalti baada ya nahodha wa Yanga Nadir Haroub kumwangusha eneo la hatari Meshack Selemani wa Prisons
                                                                                                        

No comments:

Post a Comment

PERUZI24HOURS Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.