Latest News

Alexis Tsipras, ametetea mageuzi ya ulipaji kodi Ugiriki, uchaguzi wa urais unafanyika Ufilipino na ‘Malkia wa Pembe za Ndovu’ atafika kortini leo Dar es Salaam.


Waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, ametetea mageuzi mapya ya mfumo wa ulipaji kodi na malipo ya uzeeni yaliyoidhinishwa na bunge.
Hatua hizo ni mojawapo wa masharti yanayohitajika kupata fungu zaidi la ufadhili wa kimataifa kuokoa uchumi wa taifa hilo lakini Bw Tsipras amesema mabadiliko hayo hayatawaathiri watu wengi waliostaafu.
Mawaziri wa fedha kutoka mataifa yanayotumia sarafu ya Euro wanakutana leo Jumatatu kujadili fungu hilo la malipo.

2. Uchaguzi wa urais wafanyika Ufilipino

Image copyright Reuters
Image caption Duterte ametishia kuwaua maelfu ya wahalifu
Mamilioni ya raia wa Ufilipino wanapiga kura katika uchaguzi wa urais ambao huenda ukashuhudia meya mwenye msimamo mkali akichaguliwa kuwa rais mpya wa taifa hilo. Meya huyo mwenye umri wa miaka 72, Rodrigo Duterte, amewachangamsha wapiga kura na kampeni zake zilizojaa ugomvi ikiwemo kutishia kuwauwa maelfu ya wahalifu.

3. Washukiwa wanne kushtakiwa Honduras

Image copyright Getty
Jaji mmoja nchini Honduras ameamua kuwa wanaume wanne wanaweza kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanaharakati wa mazingira, Berta Caceres.
Baadhi ya watu hao ni wanajeshi waliostaafu na wengi bado wanahudumu jeshini. Wengine wameajiriwa na kampuni zinazojenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme ambalo ujenzi wake Bi Caceres na vuguvugu la wenyeji limekuwa likipinga.

4. Seoul yapuuza pendekezo la Korea Kaskazini

Image copyright AFP
Image caption Kim amependekeza nchi hizo mbili zikutane kwa mazungumzo
Serikali ya Korea Kusini imepuuza na kulitaja kuwa propaganda ya kinafiki pendekezo la Korea Kaskazini kwamba mataifa hayo mawili yanapaswa kukutana kufanya mazungumzo.
Tamko hilo linafuatia tangazo la kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, katika kongamano la chama tawala cha Workers Party.
Lakini baadaye kongamano hilo liliidhinisha azimio linaloimarisha uwezo wa Pyongyang kujihami kwa silaha za nyuklia.

5. Wanauchumi wapinga mataifa nafuu kwa kodi

Image copyright AFP
Image caption Mkutano wa kupambana na ufisadi utafanyika baadaye wiki hii London
Zaidi ya wanauchumi 300 wametia saini barua kwa waziri mkuu wa Uingereza David Cameron pamoja na viongozi wengine duniani wakisema hakuna sababu zaidi za kuendelea kuwepo maeneo ya kuhifadhi pesa za kigeni kwa ajili ya kukwepa kulipa kodi. Ujumbe wao unakuja kabla ya mkutano wa kupambana na ufisadi mjini London baadaye wiki hii.

6. Malkia wa Pembe za Ndovu kufika kortini Tanzania

Image copyright AFP
Na mfanyibiashara mmoja wa kichina mwanamke anatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Tanzania hivi leo kufunguliwa mashtaka ya kuendesha mtandao wa kihalifu uliokuwa ukisafirisha kimagendo pembe za ndovu hadi barani Asia.
Viongozi wa mashtaka wamesema kuwa Yang Feng Glan, ambaye anajulikana kwa jina la utani kama Malkia wa pembe za ndovu aliongoza biasha haramu iliyowauwa ndovu katika mbuga za wanyama.
Amekanusha mashtaka hayo.

No comments:

Post a Comment

PERUZI24HOURS Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.