MABONDIA 12 wa Tanzania wanatarajiwa kupanda ulingo mmoja katika pambano la ngumi kuwania mkanda wa TPBC litalalofanyika kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) Chaurembo Palasa, pambano hilo litafanyika Agosti 7, mwaka huu.
Alisema pambano hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Dippo and Metro Water, litamkutanisha Karama Nyilawila dhidi ya Seleman Galile, bondia kutoka Mbeya Meshack Mwenkemwa dhidi ya bondia wa Dar es Salaam Seleman Zugo.
Palasa alisema katika pambano hilo la kukata na shoka, litawakutanisha mabondia hao wenye uwezo katika pambano la raundi 10 uzito wa kati.
Pia, Abdallah Zamba atapambana dhidi ya Haidaly Mchanjo huku Richard Nyembela akikutana na Nassoro Salum raundi sita.
Mabondia wengine ni Sweet Kalulu atakayepambana dhidi ya Abdul Zugo na Ismail Ndende atakayechuana na Msafiri Matumla. Rais huyo alisema pambano hilo linajaribu kuwapa nafasi mabondia kuonesha uwezo wao kwa ajili ya kutengeneza viwango vyao vya ubora.
No comments:
Post a Comment