Latest News

Ajuza abakwa na kuuawa


CHRISTINA Mnyira (89) mkazi wa Patandi wilayani Arumeru mkoani Arusha amekutwa amekufa baada ya kubakwa na kunyongwa shingo.
Mnyira alikutwa amekufa Julai 21 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo alisema kijana mmoja ametiwa mbaroni na mwingine anasakwa.
Alisema baada ya bibi huyo kufanyiwa unyama huo mwili wake ulitupwa katika msitu wa Chuo cha Mifugo Tengeru na wasamaria wema walitoa taarifa polisi.

No comments:

Post a Comment

PERUZI24HOURS Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.