Latest News

Sarafu ya Nigeria kushuka

Benki kuu ya Nigeria itaruhusu sarafu yake kushuka thamani kuanzia juma lijalo.

Akihutubia kwa njia ya televisheni, Gavanna wa benki kuu Godwin Emefiele amesema, thamani ya kubadilisha fedha itakuwa ikidhibitiwa.

Tangu mwezi wa Februari mwaka jana thamani ya ubadilishaji fedha ilikua ni kiasi cha naira 197 kwa dola moja ya marekani na katika masoko yasiyo rasmi gharama yake inafika mpaka karibu na Naira 350.

Hatua hiyo inakusudia kupambana na changamoto ya kukosekana kwa fedha za kigeni,kulikosababishwa na kuanguka kwa bei ya mafuta na kuvutia wawekezaji.

Lakini mwandishi wa BBC jijini Lagos anasema hali hii inaweza kusababisha kupanda kwa gharama za bidhaa na kusababisha athari kubwa kwa mamilioni ya Raia wa Nigeria wanaoishi kwenye lindi la umasikini.

No comments:

Post a Comment

PERUZI24HOURS Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.