Utawala nchini Ufaransa uko katika
hali ya tahadhari kuu baada ya mvua kubwa kunyesha katika maeneo ya
milima na kutishia kusababisha mafuriko zaidi.
Mabarabara kadha na reli na hata daraja chache zimefungwa katika maandalizi ya kupambana na mafuriko hayo yanayotarajiwa.
Tahadhari hiyo kuu inatokana na vifo vya takriban watu 10 katika siku tatu zilizopita nchini humo na Ujerumani ambayo pia imeathirika vibaya na mafuriko hayo.
Miji kadhaa Kusini mwa Ujerumani imeharibiwa sana na mafuriko.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ametaja hali ya hewa kama mabadiliko yanayohusiana na mabadiliko makubwa kote duniani.
No comments:
Post a Comment