Afrika Kusini inaadhimisha miaka 40
tangu maandamano ya wanafunzi wa Soweto, walipopinga ubaguzi wa rangi
katika elimu kwa kulazimishwa kusomeshwa kwa lugha ya Ki-Afrikaan.
Maandamano hayo yalikuwa kama mwanzo wa kuelekea hatua za kumalizwa kwa utawala wa makaburu wa Afrika Kusini.
Makamu wa rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, ameweka shada la maua kwenye kaburi la kijana Hector Pietersen.
Picha hiyo ilibua hamasa na hasira kubwa na kuufanya ulimwengu kulaani ukatili uliokuwa ukiendelezwa na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo.
No comments:
Post a Comment