Latest News

Mgombea urais wa zamani akamatwa Congo-Brazzaville


Mkuu wa zamani wa jeshi na mgombea wa kiti cha urais aliyeshindwa nchini Congo-Brazzaville amekamatwa.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwa jenerali Jean-Marie Michel Mokoko, lakini Rais Denis Sassou Nguesso amemlaumu awali kwa kupanga mapinduzi.

"Hii ni njia ya kumdhuru jenerali, ambaye alisimama na bwana Nguesso wakati wa uchaguzi uliopita," msemaji wa chama cha I'IDC-FROCAD Guy Romain Kinfouissia , aliliambia shirika la Reuters.

Bwana Sassou Nguesso ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1979, alichaguliwa tena mwezi Machi kwenye uchaguzi uliopingwa na upinzani.

No comments:

Post a Comment

PERUZI24HOURS Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.