Kenya inatuma kikosi kikubwa cha jeshi hadi katika mpaka wake na Somalia.
Nia ya kikosi hicho kikubwa kutumwa Somalia bado haijabainika, lakini kuna tetesi kuwa huenda Kenya ikarejelea mipango yake ya awali ya kujenga ukuta wa usalama kaskazini mwa nchi hiyo, mpakani na Somalia.
Taarifa za kuaminika zinasema kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili kaskazini mwa Kenya umefungwa.
Serikali ya Kenya na Somalia bado hazijasema lolote.
No comments:
Post a Comment