Latest News

Waliotaka 'kumteka' Erdogan wakamatwa Uturuki


Wanajeshi maalum wa Uturuki wamewatia mbaroni wanajeshi wanaoshukiwa kufanya jaribio la kumteka rais Recep Tayyip Erdogan wakati jaribio la mapinduzi lililotibuka, lilipoanza wiki mbili zilizopita.
Ripoti zinaarifu kwamba takriban makomando 11 walitiwa mbaroni nje ya mkahawa wa Marmaris ambapo rais Erdogan alikuwa ameenda likizoni, japo alitoweka baada ya kudokezewa kuhusu mpango huo kabla ya makomando hao kumvamia.
Maafisa wanasema ndege zisizokuwa na rubani na helikopta zilitumiwa kuwasaka watoro hao, baada ya kuonekana na wanakijiji wakiwinda ngiri katika eneo hilo la misitu.

No comments:

Post a Comment

PERUZI24HOURS Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.