TIMU za Ligi Kuu Tanzania Bara zinatarajiwa kukabidhiwa vifaa vya michezo na wadhamini wakuu wa ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya Alhamisi.
Taarifa ya Meneja Uhusiano wa Vodacom, Matina Nkurlu kwa vyombo vya habari jana ilisema hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo itafanyika Makumbusho Dar es Salaam.
Alivitaja vifaa vitakavyokabidhiwa ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, mipira, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika, vyote kwa mujibu wa mkataba.
“Vifaa vyote kwa ajili ya ligi ya msimu ujao vipo tayari kilichobakia ni kuvikabidhi siku ya Alhamisi ili timu ziweze kuendelea na maandalizi mengine kabla ya ligi kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti,” alisema.
No comments:
Post a Comment