Latest News

MFUMUKO WA BEI ZA BIDHAA WA TAIFA KWA MWEZI JANUARI. 2018

                                          DAR ES SALAAM

Ofisi ya Taifa Ya Takwimu NBS imesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa Kwa mwezi Januari 2018 umebaki kuwa asilimia 4.0 kama ilivyokuwa mwezi disemba 2017.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii EPHRAIM KWESIGABO amesema takwimu hizo zinaonesha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Januari 2018 umekuwa Sawa na kasi ya mwaka 2017.

KWESIGABO amefafanua kuwa mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi cha mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na Kaya binafsi hapa nchini.

amesema bei za baadhi za vyakula zilizochangia mfumuko wa bei kufikia asilimia 4.0 Kati ya mwezi januari 2017 hadi januari 2018 ni pamoja na mahindi ,maharage , samaki na ndizi za kupika.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS ni  taasisi ya umma iliyoanzishwa Kwa sheria ya Takwimu mwaka 2015 iliyopewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa Takwimu rasmi nchini.

                                          Na.  ASHURA DUNDA


No comments:

Post a Comment

PERUZI24HOURS Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.